Monday , 9th Feb , 2015

Halmashauri za wilaya mkoani Tanga zimeagizwa kuhakikisha kuwa zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya zinakuwa na dawa za kutosha kwa sababu hakuna sababu za msingi za kukosekana kwa huduma hiyo wakati fedha za kununulia zipo.

Agizo hilo limekuja kufuatia baadhi ya wilaya za mkoa huo kuwakatisha tamaa wananchi kujiunga katika zoezi la kitaifa la mfuko wa afya ya jamii kwa sababu ya tatizo hilo.

Agizo hilo limetolewa na mganga mkuu wa mkoa wa tanga dr,asha mahita wakati kamati ya afya mkoa ilipokutana na na waratibu wa CHF wa wilaya za Muheza na Lushoto ambazo zinaongoza kwa kufanya vibaya chini ya mpango huo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wadawa katika maeneo yanayotoa huduma hiyo.

Awali akielezea sababu kuu zilizosababisha wilaya yake kushindwa kufanya vyema katika zoezi la kujiunga na mfuko, mratibu wa CHF wa wilaya ya Lushoto Dkt Juma shetumba amesema mwanzo walipokuwa wakianza zoezi hilo baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji na kata walibainika kutumia vibaya michango ya wananchi waliokuwa wakikusanya kwa lengo la kujiunga hatua ambayo walilazimika kubadilisha utaratibu huo kwa kuwaweka vingozi hao kuwa wahamasishaji.

Kufuatia hatua hiyo katibu tawala mkoa wa Tanga Salum Chima amewataka wananchi kuachana na dhana potofu ya mfuko huo ya kudhani kuwa kiwango cha shilingi elfu 10,000/= wanachongangia kwa kila kaya ni kikubwa kwa sababu hawaugui mara kwa mara na badala yake amewataka kujiunga kwa sababu chini ya mpango huo kutaziwezesha familia zao kunufaika kwa muda mrefu na huduma za afya.

Tags: