
Hayo yamebainishwa leo Alhamisi na Meneja wa Wakala wa Barabara Dar es Salaam (Tanroads), Julius Ndyamkama ambaye amesema kwamba
“Leo tutaweka alama ya X kwenye jengo la Tanesco kwa ajili ya kuanza ubomoaji. Baada ya kuweka alama hiyo tutoa notisi ili kuwajulisha kuhusu zoezi hilo,” amesema .
Rais John Magufuli jana alitoa agizo wakati alipotembelea eneo la mradi huo mara baada ya kutua jijini Dar es Salaam akitokea Wilaya ya Chato mkoani Geita na kuwaambia wakala wa barabara nchini kubomoa jengo la Tanesco kupisha ujenzi wa mradi wa barabara za juu zinazotarajiwa kujengwa eneo la Ubungo.
Ubomoaji huo pia utahusisha ofisi za Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambazo pia zinapakana na jengo la Tanesco eneo la barabara ya Morogoro.
Hata hivyo imedaiwa kwamba Mradi huo utaigharimu Tanzania kiasi cha Sh188 bilioni.