Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wa kwanza kushoto), akiongozwa na Meneja Mwandamizi Miradi ya Umeme wa TANESCO, Gregory Chegere.
Dkt. Kalimani amesema hayo katika uzinduzi wa kituo cha udhibiti wa umeme wilayani Chato, Mkoani Geita, na kuwataka wananchi wanaopata nishati hiyo waitumie kikamilifu kwa ajili ya maendeleo yao.
Dkt. Kalimani amesema kuwa licha ya shirika hilo kuonekana kufanya vizuri katika usambazaji umeme nchini lakini bado kuna sehemu kubwa ya wananchi bado hawajafikiwa na huduma hiyo hivyo shirika hilo halinadubi kufanya jitihada kuwafikia wateja wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini Felischmi Mramba, amesema kuwa umeme kwa sasa utakuza ajira kwa wananchi hivyo amewataka wananchi hao kutunza miundombinu ya mradi huo.