Monday , 12th Oct , 2015

Shirika la umeme nchini hivi karibuni kinatarajia kuzima kituo kingine cha kuzalisha umeme cha kidatu kinachotegemea maji kutoka bwawa la mtera hivi karibuni kutokana na kuishiwa maji kwa ajili ya kuendesha mitambo hiyo

Meneja wa Tanesco kituo cha kuzalisha umeme cha kidatu Mhandisi Justus Mtolela

Meneja wa Tanesco kituo cha kuzalisha umeme cha kidatu Mhandisi Justus Mtolela amesema kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha megawati mia mbili kimepunguza uzalishaji wake hadi kufikia megawati 30 na kwamba hali hiyo inatokana na kukosekana kwa maji ya kuendeshea mitambo.

Mtolela ameongeza kuwa kina cha maji katika bwawa la Kidatu kimeshuka kutoka mita za ujazo 450 hadi kufikia mita 441 huku kiwango cha mwisho kinachoruhusiwa kuzalisha umeme kikiwa ni mita 433.

Kukauka kwa maji katika bwawa la Mtera na Kidatu ni athari inayotokana na kukauka kwa maji ya mto Ruaha Mkuu ambao ndiyo tegemeo la bwawa hilo la mtera linalohudumia pia bwawa la Kidatu kwa pamoja na mto Lukosi na Iyovi ambayo na yenyewe imekauka

Hivi karibuni baadhi ya wataalamu na wadau wa rasilimali za maji wamekuwa na maoni na mapendekezo kwa serikali juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kunusuru rasilimali hiyo na kuifanya kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kutazama upya mgawanyo wa maji kwa sekta mbalimbali na pia kusimamia ufanisi katika matumizi yake.