
Akiongea na waandishi wa habari hii leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa (TAMWA) Bi. Edda Sanga amesema kuwa TAMWA imebaini kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 jumla ya kesi 63 za ubakaji zilizoripotiwa na ni kesi moja pekee iliyotolewa hukumu mahakamani.
Aidha, ameongeza kuwa kati ya kesi 62 zilizobaki 43 bado zipo mahakamani mpaka hivi sasa, 17 hazikufika mahakamani na kesi mbili zimefutwa na kusema kuwa hata hizo kesi chache zinazoshuguhulikiwa huchukua muda mrefu kutolewa hukumu.
Kwa upande wake mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Mary Richard amesema kuwa kwa hivi sasa watu wengi hutoa taarifa mara baada ya tukio la ubakaji lakini tatizo ni kwenye vyombo vya dola ambavyo hushindwa kukusanya ushahidi kwa wakati na kusababisha kesi hizo kuchelewa kutolewa hukumu.