Wednesday , 29th Jul , 2015

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU, Dkt. Edward Hoseah amesema kuwa wamejidhatiti kikamilifu kupambana na watu wote waliojilimbikizia mali kwa njia sizizo halali kama rushwa na kutakatisha fedha.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU, Dkt. Edward Hoseah

Dkt. Hoseah ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa watumishi wote wa Takukuru nchini juu ya jinsi ya kupambana na wale wote waliojilimbikizia mali kwa njia za rushwa na kutakatisha fedha na wengine kuzificha ulaya.

Dkt. Hoseah ameongeza kuwa kitengo hiko kipo toka mwaka jana ila wamepata Mtaalamu toka Uingereza sasa ili kuwapa mbinu za kitaalamu ili kufanya kazi hiyo vizuri.

Aidha Dkt. Hosea amewataka wanasiasa wote kuepuka ruswa hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na yoyote atakayekiuka sheria za Uchaguzi cha sheria za Garama za uchaguzi atachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwasii wasicheze mchezo mchafu.