Thursday , 25th Feb , 2016

Serikali imeitaka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), kuhakikisha kwamba sekta ya hifadhi ya Jamii inawafikia Watanzania wengi zaidi hasa walio katika sekta sizizo rasmi.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na walemavu, Mhe. Jenista Muhagama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na walemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo jana wakati wa ziara yake ya kuangalia mamlaka hiyo ni jinsi gani inatekeleza sheria ya kifungu cha tano katika kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Mhe. Jenista amesema mpaka sasa Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania wengi hawajafikiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii na hasa wale walipokatika sekta isiyo rasmi na kuongeza sasa ni wajibu wa SSRA kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa watanzani wote nchini.

Aidha waziri huyo amewataka SSRA kutoa taarifa ya kazi yao ya usimamizi wa uwekezaji hasa kwa ya mifuko ya hiyo na kuona kama ina tija kwa wananchi pamoja na kuona kwamba mifuko hiyo inawezaje kutatua changamoto ya tatizo la ajira kwa vijana nchini.

Aidha ameitaka mamlaka hiyo kutoa maoni yake juu ya mfumo uliopo sasa kama unawawezesha kusimamia kikamilifu majukumu yake iliyopewa ili kuendeleza sekta na pia kutoa maoni juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa sasa kama inakidhi haja ya wakati tuliopo.