
Ndugai ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, alipokuwa akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an yaliyowashirikisha zaidi ya watoto na vijana 40 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Spika Ndugai ameeleza kuwa umoja na mshikamano uliopo hapa nchini ni matokeo ya viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini kuendelea kuhubiri amani na utulivu na kuitaka jamii na viongozi hao kuiendeleza kazi hiyo
"Waziri wa Mambo ya Ndani anafanya kazi ya kuangalia shughulia za kidini ndani ya nchi yetu zinandelea kwa amani kati ya dhehebu na dhehebu, endeleeni kuhubiri amani kila siku. Kazi iliyoifanywa na nyie Masheikh ni kubwa mno kwani kama amani mmeihubiri na tayari watanzania wameshaishika. Watanzania wanauvumilivu wa kipekee sasa inabidi kuhubiri uvumilivu wa kidini" Ndugai.