Wednesday , 11th Mar , 2015

Waziri wa Uchukuzi Mh. Samweli Sita amesisimamisha upokeaji mabehewa 124 toka nchin India mpaka taarifa ya kuchunguza tuhuma za mabewa yaliyo chini ya kiwango itakapo kabidhiwa kwake wiki ijayo.

Waziri Sita ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kukutana na bodi ya shirika la Reli nchini TRL na kuongeza kuwa Mabehewa hayo yanaonekana sio imara kwan yamekuwa yakidondoka mara kwa mara hasa kwa mwezi decemba yalikuwa yakidondoka kila siku,

Mh. Sita amesema kati ya mabehewa 274 yaliyoagizwa na kulipiwa Nusu ya garama huko nchini India mabehewa 150 yameshakuja nchini na 124 bado na kusitisha yasije mpaka atakapo kabidhiwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya mabehewa hayo yaliyo chini ya kiwango.

Sitta aliongeza kuwa zabuni ilihusisha ununuzi wa mabehewa 274 na kwamba 150 tayari yalishaingia nchini huku kukiwa na harufu ya ufisadi kuwa yalitengenezwa chini ya kiwango.

Hata hivyo sema amesema kuwa serikali ililipa asilimia 50 ya gharama zote za manunuzi na kwamba iwapo ikibainika udanganyifu wowte kampuni hiyo itawajibika.

Ripoti hiyo itakabidhiwa jumatatu ijayo kwa Mh. sita ili wahusika wote wajulikane na Wawajibishwe