
Waziri wa nchi Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene wakati akifungua mkutano wa tano wa bodi ya mfuko wa barabara,
Waziri Simbachawene, amesema kuwa barabara nyingi zilizoko katika serikali za Mitaa zinajengwa chini ya kiwango kutokana na fungu dogo la fedha ambalo linatengwa na bodi hiyo hali inayofanya barabara hizo kuharibika haraka.
Waziri Simbachawene amesema mapungufu hayo yasijitokeze tena kuanzia wakati huu na kurekebisha taratibu na utoaji fedha kwa ajili ya babaraba hizo ili zijengwe kwa kiwango bora kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na kukuza uchumi kwa haraka.
Aidha Waziri Simbachawene ametumia fursa hiyo kuwanyooshea vidole wakurugenzi wanaochelewesha malipo ya wakandarasi mara baada ya kumaliza kazi katika miradi yao.