Wednesday , 20th May , 2015

Wizara ya Fedha Zanzibar imekiri kuwa kuna haja ya kuangalia upya mfumo unaotumika katika ukusanyaji wa kodi baada ya kubaini kuwa kuna utitiri wa vyombo vinavyokusanya kodi katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Omary Yusuph Mzee mwenye tai ya Blue akiwa na Makamu wa rais wa Tanzania Dkt, Gharib Bilal na wawekezaji wa Kigeni.

Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Omary Yusuph Mzee amesema umefika wakati wa kuweka mfumo mmoja wa ukusanyaji wa mapato ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara wa Zanzibar.

Mh. Mzee amesema Taasisi zinazokusanya kodi Zanzibar ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB, Baraza la Manispaa Zanzibar, Halmashauri za Miji, Mamlaka ya mji Mkongwe na taasisi za Idara katika wizara mbalimbali.

Katika hatua nyingine amesema wafanyabiashara wadogo visiwani humo hawatozwi kodi ya ongezeko la thamani la asilimia 18 bali hutozwa kwa asilimia tatu ya ushuru wa stempu.