Tuesday , 1st Dec , 2015

Serikali kupitia wizara ya nishati na madini imetenga maeneo yenye ukubwa wa Hekta 197,432 kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud

Akizungumza jijini Dar es salaam msemaji wa wizara ya nishati na madini nchini Badra Masoud amesema kuwa wizara imekuwa ikitenga maeneo tengefu kwa ajili ya wachimbaji madini wadogo ambao ni watanzania pekee bila kuingiliwa na wawekezaji kutoka nje.

Amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia tayari imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 3.4 kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu wa fedha 2015/2016 kwaajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupatiwa ruzuku kwa awamu ya tatu ili waweze kuchimba kisasa na kuongeza vipato vyao na pato la taifa.

Wakati huo huo bi Badra amesema kuwa miili yote mitano 5 ya wachimbaji wadogo waliofukiwa kwenye mgodi wa Geita imepatikana