Friday , 6th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imesema imechelewa kuanza kuwalipa Pensheni wazee nchini kutokana na mpango huo kutokamilika, licha ya waziri mkuu kutoa agizo la kuwalipa katika sherehe za kilele cha siku ya wazee Duniani mwaka 2010.

Naibu waziri wa kazi na ajira nchini Tanzania, Makongoro Mahanga (kushoto) akizungumza na aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii Ezekiel Maige.

Hayo yameelezwa leo Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira nchini, Dkt. Makongoro Mahanga wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum Mhe. Leticia Nyerere aliyetaka kufahamu kwa nini agizo la waziri mkuu halijatekelezwa.

Dkt. Mahanga amesema maeneo ambayo maandalizi hajakamilika ni pamoja nakubaini vyanzo endelevu vya mapato vitakavyosimamia mpango huo na kuandaa chombo cha kusimamia malipo hayo kwa wazee.