Monday , 30th Nov , 2015

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini imepiga marufuku usafirishaji chumvi isiyowekwa madini joto katika mgodi wa Ngedabi huko Manyara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando.

Agizo hilo limetolewa wakati mgodi huo ukiwa na chumvi karibu tani elfu 60 za chumvi isiyo na madini joto iliyokuwa tayari kusafirishwa.

Mjumbe wa Bodi ya Udhibiti wa Madini Joto Bw. Luis Mmbando amesema ni lazima kwa wachimbaji chumvi kuboresha biashara ya chumvi kwa kuongeza madini joto ili kukuza soko lake na kuwaepusha watumiaji na madhara ya kiafya.

Katika ziara hiyo iliyowakutanisha wachimbaji Chumvi wamejaribu kuwakumbusha madhara ya kutumia madini ya madini joto ambapo kuna madhara 104 yanayotokana na ukosefu wa madini joto.

Aidha wambainisha kati ya madhara yanatokana na ukosefu wa madini joto ambapo karibu watu milioni 5 nchini Tanzania wanakabiliwa na madhara yao ni pamoja na tezi la shingo, watoto kuzaliwa na utindio wa ubongo, udumavu wa akili na mengineyo.