Thursday , 5th May , 2016

Serikali imesema kuwa muda wowote itawasilisha hati ya kuridhia mkataba wa kimataifa kuhusu haki za walemavu ili kufungua milango ya kutoa huduma na kuwafanya watu wenye ulemavu kuwa sehemu ya wachangiaji wakubwa wa shughuli za maendeleo nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi.

Hayo yamesema leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha ambaye alitaka kujua kwanini serikali bado haijapeleka hati ya ripoti Umoja wa Mataifa licha ya kuuridhia mkataba wa haki za walemavu mwaka 2006 lakini hadi leo hakuna kilichofanyika.

Mhe. Majaliwa amesema moja kati ya la kuunda wizara inayoshughulikia masuala ya Walemavu ni kuweza kuhakikisha wanakuwa na haki sawa katika shughuli mbalimbali hivyo waziri mwenye dhamana juu ya suala hilo tayari ameshaanza lishughulikia suala hilo.

Waziri Majaliwa amesema kuwa baada ya kuunda serikali ya awamu ya tano sasa watafanya mapitio ya mikataba yote ya Kimataifa ilipifikiwa na kisha kuikamilisha ukiwemo mkataba huo wa haki za walemavu.

Aidha, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtaka Naibu Waziri anaeshughulikia masuala ya Walemavu Dkt. Abdallah Possi kuanza mchakato wa kukutana na wadau ili kukusanya maoni ambayo wataweza kuyasilisha katika ukamilishaji wa mkataba huo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa