Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Maafa Zanzibar Ali Juma wakati alipofika katika kambi
Hayo yamebainishwa jana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, baada ya kutembelea kambi ya waathirika hao na kuongeza kuwa serikali inapaswa kuhakikisha wananchi wake wanaishi vizuri.
Dkt. Shein amesema kuwa serikali itahakikisha uwepo wa yale yote yaliyokuwa hayapo kwenye kituo hicho ikiwa ni pamoja na kutoa ahadi ya kuwapeleka shule watoto wenye umri wa kusoma ambao wapo katika kambi hiyo.
Aidha, rais wa Zanzibar amesema kuwa matukio hayo ya Mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika ni matokeo ya mabadiliko ya Zanzibar ambapo katika baadhi ya maeneo hakujajengwa kufuata utaratibu wa ujenzi na kusabaisha maafa pindi mvua zinaponyesha.
Wananchi wapatao 420 wapo kwenye kambi hiyo wakiwemo wanawake 240 na wanaume 180 huku watoto wadogo waliochini ya umri wa miaka mitano wakiwa 54 na wazee wapo 60 wote wanatoka katika sehemu za Kwahani,Welezo na Nyerere katika wilaya ya Mjini Unguja.