Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Wazri Mkuu wa Serikali yake Mhe. Kassim Majaliwa
Akizungumza na wakazi wa Kigoma katika mwalo wa Kibirizi, Waziri Mkuu amesema mradi huo utaambatana na ujenzi wa bandari kavu eneo la Katosho Mjini Kigoma kwa ajili ya kushusha mizigo inayosubiri kwenda nje ya nchi.
Aidha waziri Majaliwa amewataka wakazi ambao tayari wameshalipwa fidia kupisha ujenzi wa bandari kavu ya Katosho kuhama mara moja huku akiongeza uthamini bado unaendelea ili kuwalipa fidia stahiki.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema serikali itatafuta masoko ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuuza samaki na dagaa wanaovuliwa kutoka ziwa Tanganyika na kuwezesha wavuvi kujiongezea kipato hali itakayowafanya wawe na uwezo wa kununu zana bora za uvuvi.
Ameongeza kwa kuwataka wavuvi na wafanyabiashara kutumia fursa ya mwalo wa Kibirizi ambalo linapokea mazao ya uvuvi na kuyachakata kwa ajili kwa ajili ya kuingia sokoni.