Friday , 2nd Oct , 2015

Serikali imetakiwa kuweka wazi mikataba, ili kweza kushirikisha wananchi katika utumikaji wa rasilimali zilizopo nchini, na kuwafanya kuwa moja ya wamiliki wa rasilimali hizo.

Serikali imetakiwa kuweka wazi mikataba, ili kweza kushirikisha wananchi katika utumikaji wa rasilimali zilizopo nchini, na kuwafanya kuwa moja ya wamiliki wa rasilimali hizo.

Wito huo umetolewa na Mwanasheria dawati la uangalizi wa serikali kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Hussein Sengu, alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Supermix kinachorushwa na East Africa Radio.

Sengu amesema ukimya na usiri uliopo kwenye mikataba mbali mbali, ndio unaofikisha nchi pabaya, na kupelekea wananchi kulaumu serikali iliyopo madarakani.

“Serikali ijayo iweke mikataba wazi ambayo tayari ishapita, lakini itakayokuja iwe shirikishi, yani watu washirikishwe kuanzia mwanzo, wananchi wanaridhia”, alisema Sengu.

Pia Bwn. Sengu ameitaka serikali kuweka mitaala rasmi kwenye elimu inayohusu rasilimali za nchi, ili jamii iweze kutambua tuna rasilimali zipi na ngapi.

“Serikali itakayokuja itengeneze pia mitaala mbayo mashuleni watu wataanza kusoma rasilimali, kuwe na somo la rasilimali, nchi yetu ina rasilimali gani, inaweza ikachangia kiasi gani, watu wakiwa na uelewa wanaweza kuona wanamiliki rasilimali zao, ukimya na usiri ndio unatufikisha hapa pabaya”, alisema Sengu.

Pamoja na hayo Bwn. Sengu amesema iwapo mikataba hiyo haitawekwa wazi na kushirikishwa wananchi kutakuwa na sababu za kifisadi, hali ambayo italeta mgogoro kwa jamii.