.jpg?itok=fV3-vtpc×tamp=1478254621)
Watoto wakipatiwa chanjo
Akichangia mada kuhusu hali ya dawa Bungeni Mjini Dodoma Waziri Kivuli wa Afya Mhe. Godfrey Mollel, amesema kuwa serikali pia inatakiwa kuweka bayana ni vipi watawasaidia wananchi pindi watakapobainika wamepata madhara kutokana na kukosa chanjo kwa wakati.
Mhe. Mollel licha ya serikali kutenga bajeti kwa ajili ya kupelekea dawa mahospitali pamoja na kusogeza maduka ya dawa kwenye hospitali za mikoa lakini bado imeoneka kuna changamoto ya bajeti katika kufikisha dawa kwa wakati.
Aidha Mhe. Mollel ameongeza kuwa fedha bilioni 28 zilizopelekwa kwa ajili ya dawa mahospitalini ni kiasi kidogo kwa robo ya kwanza kulingana na mahitaji ya dawa zinazohitajika katika mahospitali.