Sunday , 8th Jul , 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kununua madeni yaliyosababishwa na mikopo ya kibenki kwenye vyama vikuu vya ushirika nchini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani, ambapo amesema anazo taarifa kuwepo kwa vyama vya ushirika vinavyokopa ili vilipe deni.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya tano inasisitiza masuala ya ushirika kwa sababu imeamua kuwahudumia wananchi kuanzia kuanzia pembejeo, dawa hadi masoko.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema mfumo wa ushirika bado unakabiliwa na changamoto ya upotoshaji na amewaagiza Maafisa Ushirika wakasimamie suala hilo kwa kutoa taarifa sahihi kwa wakulima.