
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
Waziri Mbarawa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa 10 uliowakutanisha wataalamu na wadau wa sekta ya uchukuzi na usafirishaji kutoka nje na ndani ya nchi kujadili namna ambavyo sekta hiyo itachochea maendeleo.
“Mkutano huu ni wamuhimu kwa sekta hii, kwani mapendekezo yalitolewa katika mkutano 9 ndiyo yalichochea serikali kununua ndege 2 za shirika la ndege Tanzania ATCL hivyo ni imani yangu kuwa mapendekezo ya mkutano wa 10 pia italenga kuonesha mapungufu na namna ya kuboresha ili kufikia mafanikio ambalo ndilo lengo letu sote” amesema.
Naye mwakilishi mkazi wa benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB Bi. Tonia Kandiero amesema, Benki ya maendeleo ya Afrika inajikita kufadhili miradi ya barabara ya barabara ikiamini kuwa usafirishaji nikichocheo cha maendeleo na kukuza uchumi.