Monday , 21st Jul , 2014

Serikali ya Tanzania imewataka wakuu wa Mikoa na makatibu tawala kuwa na mahusiano mazuri na kuepuka muingiliano wa kiutendaji ili kusaidia kutekeleza majukumu waliyopangiwa.

Makamu wa pili wa rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala amesema kuwa muingiliano huo umesababisha watendaji hao kutofanya kazi kwa ufanisi.

Balozi Iddi, amesema kuwa bado mikoa inakabiliwa na changamoto za usimamizi kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo ndizo msingi wa kutoa huduma bora kwa wananchi, na kufafanua kuwa mawasiliano mazuri baina ya katibu tawala na mkuu wa mkoa yatasaidia katika kutafuta ufumbuzi kwa pamoja.

Naye Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadik amekiri kuwepo kwa changamoto za muingiliano wa kiutendaji miongoni mwa pande hizo mbili , na kueleza kuwa mafunzo hayo yataboresha uhusiano katika uwajibikaji.