Monday , 18th Apr , 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu leo amezindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mwenge wa Uhuru mwaka huu unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri za wilaya na Manispaa zipatazo 179 za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kazi ya kuzindua mbio hizo imepambwa na shamrashamra za halaiki kutoka kwa vijana zaidi ya 1,000 na vikundi vya utamaduni kutoka wilaya za Morogoro na nje ya mkoa huo.

Baada ya kuwashwa leo, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kuhitimishwa wilayani Gairo ambako Aprili 25, mwaka huu utakabidhiwa mpakani mwa wilaya hiyo na Kilindi ya Mkoa wa Tanga ili kuendelea na mbio zake.

Aidha kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu ni George Jackson Mbijima kutoka mkoani Mbeya ambapo atakimbiza Mqwenge huo nchi nzima na kilele chake ni Oktoba 14, mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu.