
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe. Jenista Muhagama.
Akizungumza na vikundi vya ujasiriamali wanawake na vijana wa wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa, Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira, na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kutowafumbia macho maofisa hao.
Mhe. Mhagama amesema kuwa Saccos zenye matatizo ya kiutendaji zinashindwa kunufaika na mikopo inayotolewa na taasisis mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea mitaji kwa sababu ya kushindwa kupata msaada kutoka kwa maofisa ushirika wa maeneo husika.
Waziri huyo amesema kuwa serikali imelenga kuwatoa vijana mitaani hivyo inataka kuona kunakuwepo na vikundi vya wajasiriamali vyenye dhamira ya dhati ya kijiletea maendeleo na kuwaondoa katika umasikini.
Aidha Mhe. Mhagama ameziagiza halmashauri kuhakikisha zinatenga maeneo yatakayotumiwa na vijana kwa ajili ya biashara au shughuli zao zingine za maendeleo.