
Rais huyo alikuwa akizungumza kuhusu mpango wa kusitisha mazungumzo kuhusu uanachama wa Uturuki katika Umoja wa Ulaya..
Umoja huo umeshangazwa na hatua anazochukua Rais Erdogan dhidi ya wale waliojaribu kuipindua serikali yake. Julai mwaka huu..
Idadi ya wahamiaji wanaoelekea katika kisiwa cha Ugiriki imeshuka tangu makubaliano ya EU na Uturuki mnamo mwezi Machi kukabiliana na idadi hiyo.
Rais Erdogan ameushutumu umoja huo kwa kuvunja ahadi yake.
Katika makubaliano hayo ,Uturuki iliahidiwa msaada, raia wake kuingia Ulaya bila Visa pamoja na mazungumzo ya kujumuishwa katika EU.