Jacob Zuma
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, uamuzi huo ni chini ya makubaliano yaliyofikiwa na wanaompinga ndani ya ANC ambapo pia yatatoa nafasi kwa Waziri wa Fedha, Pravin Gordhan, kuachia ngazi.
Mvutano ndani ya chama hicho uliongezeka wiki hii baada ya Rais Zuma kumuamuru Bw. Gordhan kurudi nyumbani kutoka nchini Uingereza alikokwenda kwa ajili ya mkutano wa uwekezaji kitendo kilichozua hisia kwamba anapanga kumtimua waziri huyo wa fedha.



