Monday , 22nd Jul , 2019

Mwanasheria wa mkali wa muziki wa RnB duniani R.Kelly aitwae Stive Greenberg, amesema R Kelly anahitaji Computer ili kukamilisha Album yake huku akiwa jela.

Mwanasheria huyo amesema msanii huyo anahitaji kitendea kazi hicho ili kumalizia Album yake ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa muda mrefu.

"Mteja wangu anahitaji kutengeneza pesa na pia alikuwa amezuiliwa kutumia Computer kwa sababu yupo katika matatizo ya kisheria, ila kwa sasa anahitaji ili kukamilisha album yake."

R.Kelly yupo jela kwa sasa na amenyimwa dhamana na anatarajiwa kupandishwa kizimbani siku sijazo baada ya kushtakiwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, kuwarekodi watoto picha na video za ngono na kosa la kushambulia kingono.