Sunday , 25th May , 2014

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia vijana sita linalowatuhumu kuwa ni viongozi wa makundi ya kihalifu, likiwemo la Panya Road au maarufu kama Mmbwa Mwitu.

Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Suleiman Kova.

Mkuu wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna wa polisi Suleiman Kova amewataja wanaowashikilia kuwa ni Athuman Saidi, Joseph Ponela, Clemence Peter na Roman Vitus ambao wote ni wakazi wa Kigogo.

Wengine ni Mwinshehe Adam ambaye ni mkazi wa Temeke Mashine ya maji pamoja na Daniel Peter ambaye ni mkazi wa Yombo, ambapo kwa mujibu wa kamanda Kova, polisi wamesambazwa katika maeneo yote kuhakikisha kuwa uhalifu unaofanywa na makundi hayo ya kihalifu unadhibitiwa.