Friday , 9th May , 2014

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, amesema hadhani kuwa lugha za kejeli na matusi zilizotolewa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ndio sababu ya wajumbe wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia vikao vya bunge hilo.

Baadhi ya viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi wakiwa katika moja ya mikutano yao na vyombo vya habari.

Mhe. Pinda ametoa kauli hiyo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akihitimisha majadiliano ya makadirio ya bajeti ya ofisi yake, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Ofisi ya Bunge, mjadala ambao jumla ya wabunge 150 walichangia.

Aidha, Waziri Mkuu Mhe. Pinda alichukua fursa hiyo kuwasihi viongozi wanaounda kundi la UKAWA kukubali kufanya mazungumzo ili kufanikisha wao kurudi katika vikao vya bunge Maalum la Katiba.