Thursday , 9th Jun , 2016

Mbunge wa Korogwe Vijijini Steven Hillary Ngonyani 'Maji Marefu' amesema anaunga mkono hatua ya serikali kuongeza kodi kwa watu wote wanaoweka majina yao kama 'Plate Number' ili fedha hizo zisaidie wananchi wengine.

Ngonyani ameyasema hayo baada ya hotuba ya Waziri wa fedha Philip Mpango kuonyesha kwamba kwa watu wanaotaka majina yao yawe Plate Number watalipia milioni 10 kama kodi kutoka milioni 5 za awali.

Ngonyani amesikika katika kipindi cha EADRIVE kinachorushwa na East Africa Radio akisema ''Mimi naona ni kitu cha kawaida kwa kuwa haiingiliani na namba za serikali hivyo hata wangeweka milioni 20 ni sawa tu ili kuwafanya vijana wanaotaka umaridadi waweze kuchangia serikali''

Aidha Mbunge huyo ameipongeza serikali kwa bajeti nzuri ambayo amesema imegusa maisha ya watu wa chini kwa kujali miradi ya barabara, reli, ndege na bandari.