Tuesday , 8th Nov , 2016

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Maji. Mifugo na Uvuvi Dkt. Marry Nagu ametoa wito kwa mashirika yanayojihususha na utoaji elimu ya utunzaji mazingira kufanya utafiti kwani baadhi ya wavuvi wanang'ang'ania kufanya uvuvi haramu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Maji, Mifugo na Uvuvi Dkt. Marry Nagu.

 

Dkt. Marry Nagu ametoa kauli hiyo mkoani Dodoma wakati wa semina iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira ya mito, bahari na maziwa.

Mwenyekiti huyo wa kamati amesema kuwa watafiti hao wanapaswa kujiuliza ni kwanini ni Tanzania peke yake ndiyo kunapatikana zana za uvivu haramu wakati katika nchi nyingine duniani ni nadra kuzikuta.

Kwa upande wako wataalamu hao wa masuala ya mazingira wakiwemo kutoka shirika la WWF. Wamesema kuwa suala la kukomesha vitendo hivyo ni vyema serikali ikawawezesha wavuvi hao kwa vyombo vya kisasa kwa ajili ya kwenda kuvua bahari kuu ili kuliingizia taifa pato.