Hayo yamebainishwa Bungeni na Mbunge wa Tabora Mjini Emmanueli Mwakasaka alipokuwa akichangia hotuba ya Rais Dkt.Magufuli katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
''Mheshimiwa Naibu Spika nataka waziri anaehusika na viwanda tukimaliza Bunge tuambatane kwenda Tabora akajionee wawekezaji wa nchi hii, kule kwangu mwekezaji amefunga kiwanda cha nyuzi na kuondoka''
''Nimefanya ziara katika kiwanda kile nimekuta kimefungwa nikauliza ufunguo uko wapi kuangalia kama mashine zinafanya kazi nikaambiwa mwekezaji aliuza kama vyuma chakavu''. Amesisitiza Mwakasaka
