Tuesday , 8th Dec , 2015

JESHI la polisi mkoani Njombe linamsaka mwalimu wa shule la msingi Kimbembe wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa tuhuma za kubaka wanafunzi wanne wa shule hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbrod Mtafungwa

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Wilbroad Mtafungwa, amesema kuwa jeshi hilo linamtafuta mwalimu Abuit Eliakimu, ambaye alikimbia baada ya kupelekwa kwa mtendaji wa kijiji hicho.

Kamanda Mtafungwa ameongeza kuwa wanafunzi hao walipohojiwa na jeshi hilo walikiri kubakwa na mwalimu huyo, na kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuona kama wanafunzi hao walipata magonjwa ya ngono.

Aidha Kamanda Mtafungwa amesema kuwa pia mwalimu huyo alipohojiwa na kamati ya shule alikiri kufanya tukio hilo na kuomba msamaha hata hivyo kamati ya shule walimkabidhi mwalimu huyo kwa afisa mtendaji wa Kinyirembe aitwaye Godfrey Mwangoka.