
Prof Mbarawa ametoa kauli hiyo leo mara baada ya kukagua maendeleo ya matengenezo ya kivuko cha Mv Magogoni na ujenzi wa vivuko vipya vya New Magogoni na na Pangani n akueleza kufurahishwa kwake kwa vivuko hivyo kutengenezwa hapahaopa nchini nTanzania.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa ufundi Umeme Nchihi Tanzanai TEMESA mhandisi Le Kujan Manase amemweleza Prof Mbarawa kuwa kazi zote za ukarabati wa injini na mitambo ya kuendeshea kivuko yanafanywa na mafundi wa TEMESA na ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa nane.
Kukamilika kwa vivuko hivyo vitatu kutaiwezesha TEMESA kuwa na vivuko 30 vinavyotoa huduma hapa nchini na hivyo kuboresha huduma ya uvushaji abiria katika maeneo mbalimbali nchini.
