Tuesday , 7th Jun , 2016

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemteua mkewe Janet Museveni kuwa waziri wa elimu na michezo katika orodha mpya ya baraza la mawaziri alilotangaza.

Katika baraza hilo lenye mawaziri 49 wengi ni wale wale na wapya wachache ikiwemo safu yake ya juu ya Makamu wa Urais na Waziri Mkuu isipokuwa kwa Manaibu waziri Mkuu ambapo awali walikuwa watatu lakini amekeua wawili tu.

Rais Museveni pia amemteua mpinzani wake katika masuala ya kisiasa Bi Betty Oliva Famya kutoka chama cha Uganda Federal Alliance aliewahi kugombea Urais mwaka 2012 na kushindwa na awamu hii pia iliyomalizika ya Uchaguzi aligombea Ubunge na kushindwa , amemteua kuwa Waziri wa Wizara Mpya ya kushughulikia masuala ya Jiji la Kampala .

Mke wake Mama Janeth Kadaha Museven amemteua kuwa Waziri wa Elimu Wakati akiapishwa kama Rais Museveni alisema huu ni muhula wa kazi na kwa hivyo baraza hili lina kazi kubwa ya kupamba na ufisadi uilokithiri nchini humo

Aidha wakati hayo yanaendelea kiongozi wa upinzani nchini humo Dkt. Kizza Besigye yupo gerezani akisubiri hukumu yake kwa kosa la uhaini kwa kujiapisha mwenyewe kuwa Rais wa nchi hiyo kinyume na katiba.