Wednesday , 23rd Mar , 2016

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha Ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Felix Ntibenda imewataka wakazi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano kwa mtu aliehusika na wizi wa mtoto wa siku tatu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Mkoa huo, Felix Ntibenda.

Ttukio hilo limetokea Mkoani humo katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru baada ya mama wa mtoto huyo kufikishwa katika Hospitali hapo akiwa amepoteza fahamu akitokea katika kijiji cha Sokoro katika wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Arusha, Bw, Ntibenda amesema mama huyo Sinyati Lucas alifikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, akiwa mahututi akiambata na watu watatu, akiwemo Mume wake, Lucas Ngaraha, na wakati akipatiwa matibabu ndipo mtoto wake huyo alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Mkuu huyo wa mkoa amesema Polisi inaendelea kuwahoji watu hao watatu ambao ni Mama Mkwe wa mama mtoto,Mkunga aliemzalisha Nyumbani pamoja mume wa mama huyo ambae wakati mke wake akipatiwa matibabu alitoweka na baadae kurejea na mwanamke ambaye alikua karibu sana na mgonjwa huyo lakini nae alitoweka katika mazingira yasiyoeleweka.

Kamanda Ntibenda amesema kuwa polisi wameshaanza mahojiaono ya kina juu ya tukio hilo na kusema kuwa endapo atabainika basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.