
Wizara ya Kilimo, mifugo na uvuvi nchini Tanzania imesema kuwa isingependa kuona kuwa kuna nyama ya kuku inayoingizwa kwa mapakiti nchini Tanzania wakati kuna viwanda vingi vya kuzalisha na kutayarisha kitoweo cha kuku nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa na naibu waziri wa wizara hiyo Mh. William Tate Olenasha wakati akiongea na wadau wa viwanda vya kuzalisha na kutayarisha kitoweo cha kuku nchini Tanzania kiwanda kimoja cha kuku jijini Dar es salaam.
Mh. Nasha amesema kuwa kazi kubwa ya wizara yake ni kukuza na kuendeleza sekta ya mifugo, kilimo na uvuvi hivyo kuendelea kuingia kwa bidhaa za aina hiyo ni kuonesha kuwa wizara yake haifuatilii maendeleo na kazi za wizara.
Aidha Olenasha amesema kuwa wafugaji wa nchini Tanzania waboreshe ufugaji na utayarishaji wa kitoweo cha kuku ili kujihakikishia soko ambalo kwa sasa limeendelea kuruhusu mianya ya watu kuingiza bidhaa hiyo hapa nchini kutokana na wafugaji wa hapa nchini kutokuwa washindani.