Ruth Minja - Mtakwimu Mkuu NBS
Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es salaam na mtakwimu mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Februari na kuongeza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya upatikanaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Februari 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upatikanaji ilivyokua kwa mwaka ulioisha Januari.
Amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 93 na senti 48 kwa mwezi Februari.


