.jpg?itok=FUYYfkVU×tamp=1478621812)
Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja (kulia) akizungumza na wanahabari hawapo pichani
Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja, amewaambia wanahabari jijini Dar es Salaam leo kuwa uwezo wa shilingi katika manunuzi umeshuka na kufikia shilingi 96 na senti 92 ikilinganishwa na shilingi 97 na senti 04 hapo mwezi Septemba.
Aidha, Mtakwimu huyo Mkuu amesema mfumuko wa bei nchini haujatofautiana sana na ule wa nchi za jirani za Kenya na Uganda ambapo nchini Kenya mfumuko umeongezeka kidogo na kufikia asilimia 6.47 kutoka asilimia 6.34 wakati nchini Uganda mfumuko umepungua kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.1 mwezi Septemba.