Thursday , 12th May , 2016

Mawakala wa ugawaji wa pembejeo za zao la korosho nchini wametakiwa kutenda haki kwa wakulima na kuacha kufanya kazi hiyo kwa ajili ya masilahi yao na watakaefanya hivyo serikali itawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafilisi mali zao na kuwafunga.

Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.

Hayo yameelezwa na mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, wakati wa uzinduzi wa ugawaji na uhamasishaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho msimu wa kilimo wa 2016/2017, uliofanyika wilayani Tandahimba, na kusema kuwa mawakala hao wanakwepa kufanya kazi na serikali za vijiji.

Aidha, amewataka wadau wa zao hilo kushirikiana na viongozi wa Bodi ya Korosho ya Korosho Tanzania (CBT), na viongozi wa serikali katika kuwapiga vita watu wachache wanaosambaza propaganda kuwaaminisha wakulima kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani haufai.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Anna Abdallah, amesisitiza kwa wakulima kutekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, la kuvitaka vijiji kupanda miche 5,000 na kila kaya angalau walime heka moja ya korosho.

Sauti ya Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, Bodi ya Korosho ya Korosho Tanzania (CBT),