
Dkt Abel Kinyondo
Pia Tanzania kama nchi inapaswa kuchukua tahadhari kubwa ya jinsi inavyosimamia sekta ya madini ili isije kuwa balaa kwa uchumi na taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi wa tafiti za kimkakati kutoka asasi ya utafiti ya (REPOA), Dkt. Abel Alfred Kinyondo, amesema hayo leo na kutaja moja ya athari hizo kuwa ni ile inayojulikana kitaalam kama Dutch Disease Effect ambapo kutokana na fedha za mkupuo na za haraka, watu huacha uzalishaji katika sekta nyingine na kukimbilia kwenye madini ambako mafuta na gesi vinapatikana na hivyo nguvu kazi yote kuhamia kwenye sekta moja ya uchumi.
Aidha, Dkt Kinyondo ametaja athari nyingine kuwa ni ya baadhi ya wanasiasa wasio waadilifu kutaka kutumia mapato ya madini kama mtaji wao wa kutaka waendelee kubaki madarakani kisiasa na kwamba kwa Tanzania inabidi wawe waangalifu dhidi ya athari hizo kwani taarifa zinaonyesha mchango utakaotokana na kuvunwa kwa rasilimali ya mafuta na gesi kwenye pato la taifa siyo mkubwa sana kama ilivyo matarajio ya wengi.