Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mapacha walioungana waaga dunia

Thursday , 17th Aug , 2017

Mapacha walioungana kuanzia kifuani hadi tumboni wamefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam walipokuwa wakipatiwa matibabu baada ya kuzaliwa katika hospitali ya Berege wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Afisa uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Neema Mwangomo amethibitisha kufariki kwa watoto hao ambao walikuwa wakisubiri kufanyiwa upasuaji, huku akisema kuwa uchunguzi unafanyika kubaini chanzo cha kifo cha watoto hao.

Watoto hao waliozaliwa wakiwa na uzito wa kilo nne walipewa rufaa ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kupatiwa uangalizi zaidi na waliwasili katika hospitali hiyo Juni 24 na kuwekwa katika chumba cha uangalizi maalum.

Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto, Dkt. Zaituni Buhari Agosti 2 mwaka huu alieleza wanahabari kuwa  watoto hao walikuwa wanachangia ini na sehemu ndogo ya moyo lakini wangeweza kufanyiwa upasuaji.

Hata hivyo baadhi ya mapacha wa aina hiyo ambao hawajawahi kufanyiwa upasuaji na kufanikiwa kuishi na kuwa watu wazima ni pamoja wale wanaoishi wilayani Kilolo mkoani Iringa na wamehitimu kidato cha sita mwaka huu na kupata ufaulu mzuri wa kuendelea na elimu ya juu..

 

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP