Monday , 26th Sep , 2016

Baraza la Usalama Barabarani nchini Tanzania, na wadau wengine wa usalama barabarani wameweka mikakati mbalimbali kupunguza ajali za zitokanazo na makosa ya binadamu ambayo huchangia asilimia 80 ya vyanzo vyote vya ajali za barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.

Akizungumza katika ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Usalama Barabarani yaliyofanyika mkoani Geita, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kuwa baraza litaweka mkazo kupambana na ajali hizo pamoja na zile zinazosababishwa na mfumo pamoja na ufinyu wa bajeti.

Kamanda Mpinga amesema kuwa wataendelea kusisitiza kukomesha makosa kwa makubwa ambayo yanapelekea vifo vingi katika ajili za barabarani makosa hayo ikiwa ni pamoja na mwendo kasi, Ulevi, kutovaa kofia ngumu, kufunga mkanda na vifaa vya kuwalinda watoto ndani ya gari.

Aidha mwenyekiti huyo wa Baraza la Usalama Barabarani, amesema kuwa kampeni yao ya kutoa mafunzo maeneo mbalimbali inasababishwa na ufinyu wa bajeti hali inayofanya washindwe kuendana na kasi ya matukio ya ajali hizi za barabarani.