Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba.
Akitangaza hukumu hiyo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Simba amesema makampuni hayo yatalipa million 25 kila moja kwa kosa la kushindwa kuwalinda wateja wake na kusababisha matapeli kutumia makampuni yako kuwachukulia fedha wateja kwa udanganyifu kupitia huduma zao za kifedha.
Dkt. Simba ameongeza kuwa faini hiyo italipwa mara moja na kama mamlaka ikipokea malalamiko zaidi toka kwa wananchi Mamlaka itawachukulia hatua kali zaidi kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wa Mwanasheri wa (TCRA), bi. Elizabeth Nzagi amewataka wananchi kuwa waangalifu pindi wanapoombwa msaada wa fedha na ndugu zao kwa kuhakikisha kuwa wanaowaomba fedha ni ndugu zao na sio vinginevyo.