
Waziri Mkuu ameyasema hayo Bungeni wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge ambapo Mbunge wa Manginga Mjini Cosota Chumi (CCM) aliyetaka kujua kauli ya serikali baada ya wananchi kupata hofu baada ya kutoka kwa tangazo la kusitishwa kwa ajira mpya.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Majaliwa amesema kwamba lengo la serikali ni jema na ajira hazitatolewa kwa muda uliotangazwa usiozidi miezi miwili ili kuhakikisha watumishi hewa wanaondolewa na kubakia watumishi halali.
''Serikali imesitisha ajirab na kupandisha vyeo ili tutakapo ajiri watu waweze kulipwa kulingana ka kazi watakazopangiwa , hivyo serikali inajipanga vizuri na baada ya hapo ajira zitatoka.''-Amesema Waziri Mkuu.
Aidha Waziri Mkuu amewataka wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidiii ili kutimiza malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.