Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa jana jijini Dar es salaam imesema kutambuliwa kwa mahujaji kumefanya idadi ya mahujaji waliofariki hadi sasa kufikia 25.
Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa hadi sasa mahujaji 15 kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta zinaendelea huku wakisema miili ya mahujaji hao imeshazikwa nchini humo.
Majina ya mahujaji hao waliotambuliwa kufariki dunia ni Faiza Ahmed Omar na Rehema Ausi Rubaga kutoka kikundi cha Khidimat Islamiya na Masoud Juma Khamis kutoka kikundi cha Ahlu Dawaaa.