Monday , 12th Mar , 2018

Daktari wa wanyama nchini Tanzania, Dkt. Obed Kiariro amedai kuna uwezekano mkubwa wa binadamu kupata ugonjwa wa vipele unaotokana na virusi vinavyotoka kwa mbwa ambao hawapewi matunzo mazuri na wale wengine wanaozurura mitaani.

Dkt. Kiariro ameeleza hayo kupitia kipindi cha Supamix kinachorushwa na East Afrika Radio baada ya siku za hivi karibuni baada ya baadhi ya watu kupenda kukaa na mbwa karibu huku wengine kushinda nao mpaka katika vyumba vyao vya kupumzikia 'setting room' bila ya kuenda kuwapa tiba mbadala za magonjwa mbalimbali ambayo anayokuwa nayo wanyama hao.

"Kuna baadhi ya virusi 'lava' wanaotokana na minyoo, ambapo unapoenda kuogelea kule maeneo ya 'beach' baharini unakuta wanapanda kwenye ngozi kisha wanaichana na kuingia ndani yake na kusababisha upele na baadae zinatengeneza vidonda. Hivi virusi vinatoka moja kwa moja kwa mbwa na hauwezi kuviona kwa macho ya kawaida kutokana na hali ya mazingira yalivyo", amesema Dkt. Kiariro.

Mtazame hapa chini Dkt. Kiariro akielezea mengine mengi kuhusiana na madhara ya kiafya yanatoka kwa wanyama ambao hawapewi matunzo stahiki.