Wednesday , 14th May , 2014

Kamati ya katiba ya kituo cha sheria na haki za binadamu imezitaka pande zinazopingana katika bunge maalumu la katiba kuridhiana katika vipengele ndani ya rasimu ya pili ya katiba mpya.

Mkurugenzi mkuu wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, Dkt Hellen Kijjo-Bisimba.

Mjumbe wa kamati hiyo mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt James Jesse amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati kamati hiyo ikitoa ripoti ya mwelekeo wa bunge maalumu la katiba ambalo kwa sasa lipo katika mapumziko mafupi kupisha bunge la bajeti.

Dkt Jesse amefafanua kuwa maridhiano yanaweza kufikiwa baina ya pande hizo iwapo wajumbe wa UKAWA watakubaliana na wenzao kutoka chama tawala CCM, juu ya vipengele tata ndani ya rasimu hiyo, hasa suala la muundo wa muungano kwa kila upande kukubali kulegeza msimamo wake kuhusu kipengele hicho.