Akiongea katika kiwanda cha urafiki jijini Dar es salaam Mwanasheria mkuu wa TUICO Noel Nchimbi amesema kuwa wafanyakazi katika kiwanda hiko wanamalalamiko makubwa ya kutokulipwa stahiki zao kwa zaidi ya miaka 7 sasa wakiwa wanadai zaidi ya bilioni 9 na mahakama iliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuwalipa fida hizo.
Kwa upande wao wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki wamebainisha kuwa kwa muda mrefu wameshinikiza uongozi wa kiwanda hiko kuwalipa stahiki zao bila mafanikio yoyote na kuchukua uamuzi wa kugoma ili wapate nafasi ya kusikilizwa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya kinondoni Paul Makonda ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanawalipa wafanyakazi hao stahiki zao ifikapo desemba moja mwaka huu. "Na kuwataka wafanyakazi wa kiwanda hiko kuendelea na shughuli za uzalishaji kama kawaida huku malalamiko yaoyakiendelea kufanyiwa kazi" alisema