Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kesi kupinga sheria mpya ya habari yafunguliwa

Wednesday , 11th Jan , 2017

Baraza la Habari Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wamefungua kesi kupinga baadhi ya vipengele vya Sheria ya Huduma za Vyombo Vya Habari ya 2016.

Kajubi Mukajanga - Katibu Mtendaji wa MCT

Kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ), ambayo ofisi zake ziko katika jengo la Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam chini ya mawakili Fulgence Massawe, Donald Deya, Jenerali Ulimwengu, Jebra Kambole, Francis Stolla na Mpale Mpoki ambao wanaziwakilisha taasisi hizo.

Katika kesi hiyo, washirika hao wanataka baadhi ya vifungu kwenye sheria hiyo ambavyo vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza vifutwe kwa madai kuwa vinakiuka matakwa ya mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ibara za 6(d) na 7(2).

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mkajanga amesema kwa mujibu wa kifungu cha 8 (1) c , Tanzania inapaswa kuchukua hatua kuhakikisha haki zote zinazotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa.

Amesema Tanzania iliridhia mkataba huo Julai 7, 2000 chini ya kifungu namba 23 cha mkataba huo, mahakama imepewa mamlaka ya kutafsiri mkataba huo na kuhakikisha nchi wanachama wanaufuata na kuusimamia.

Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge Novemba 5 mwaka jana na baadaye kuidhinishwa na Rais Magufuli Novemba 16 mwaka jana.

Wasikilize hapa, Kajubi (MCT), Bi Helleni Kijo Bisimba (LHRC) na Onesmo Olengurumwa (THRDC)

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP